Miongozo ya Jumuia

Chat & Date ni mahali pa kuchumbiana kwa uaminifu. Ni mahali ambapo kila mtu anaweza kuonesha uhalisia wake kuhusu yeye ni nani na anatafuta nini.

Tunataka kila mtu afurahie safari yake kwenye Chat & Date, na kutumia jukwaa letu kwa usalama na uwajibikaji. Mamilioni ya watu ulimwenguni kote wanatutegemea sisi tudumishe nafasi salama na ya kuaminika wanapotengeza mahusiano mapya. Tumeunda miongozo hii ya jumuia ili kukusaidia uelewe ni tabia gani inakubalika na tabia gani haikubaliki kabisa katika jukwaa letu.

Sera zetu zinatengenezwa kwa msaada wa jumuia yetu na kujitolea kwa wafanyakazi wetu kudumisha nafasi salama ili kutengeneza mahusiano mapya.

Tumejitolea kuzipitia tena na tena sera zetu bila kuacha ili ziweze kuhusisha na kuwakilisha utofauti wenye namnaamna ya wanajumuia wetu, na kwenda sambamba na mabadiliko mengi yanayotokea ulimwenguni.

Chat & Date si mahali kwa ajili ya:

Watoto

Chat & Date ni jukwaa la watu wazima tu. Hii inamaanisha kwamba lazima uwe na umri wa miaka 18 au zaidi ili ujiunge na jukwaa hili. Ikiwa tunapata ushahidi wowote unaothibitisha kwamba unaweza kuwa chini ya umri, tutakuzuia ili usipate huduma hii. Ikiwa tumefanya hivyo kimakosa, tuna haki ya kukuomba kitambulisho ili kuthibitisha umri wako.

Tunaelewa kwamba baadhi ya wanajumuia wangependa kujumuisha watoto kwenye picha zao. Tunaomba watoto wasionekane peke yao kwenye picha na wakiwepo wawe wamevalishwa mavazi kikamilifu. Hii ni kwa ajili ya usalama wa kila mtu anayehusika.

kwa ufupi:

 • Hakuna mshiriki mwenye umri chini ya miaka 18.
 • Hakuna picha za watoto peke yao katika wasifu wako.

Wasifu Bandia

Unapojiunga na Chat & Date, tunatarajia uwe mwaminifu na mkweli. Hiyo inamaanisha lazima: utumie jina unalotumia katika maisha ya kila siku, tumia tu picha zako halisi, usijioneshe kwa njia isiyokuwakilisha wewe au kujifanya mtu mwingine, au kubadili taarifa zozote kukuhusu.

Hilo linahusisha:

 • Kusema uwongo kuhusu taarifa zako zikiwemo umri na mahali unapoishi.
 • Kupakia au kutuma picha ambazo hazikuoneshi wewe.
 • Kupakia au kutuma picha zilizotengenezwa ambazo zinaashiria kuwa ni mtu mwingine.
 • Kupakia picha ambazo uso wako umefichwa.
 • Kupakia picha ambazo zina alama ya maji, nembo, zimezibwa na maandishi au kuhaririwa sana.

Ubaguzi

Sisi ni jumuiya yenye watu wa jamii tofauti tofauti. Hii inamaanisha wakati wote unapaswa kuheshimu imani, masilahi na utambulisho wa watu wengine. Chat & Date inachukua msimamo mkali dhidi ya matamshi ya chuki na ubaguzi.

Tunachukulia maudhui kuwa matamshi ya chuki (na tunachukua hatua kali zaidi dhidi ya wasifu) ikiwa yanachochea au kuunga mkono ubaguzi wa rangi, msimamo mkali, ujeuri, chuki, udhalilishaji, au madhara dhidi ya watu binafsi au vikundi kwa kutegemea:

 • Rangi
 • Kabila
 • Ulemavu
 • Umri
 • Utaifa
 • Uvutio wa kimapenzi
 • Jinsia
 • Utambulisho wa jinsia
 • Dini
 • Mwonekano (ikiwemo uaibishaji)

Hii inahusisha:

 • Alama zinazowakilisha vikundi vya chuki au imani za kibaguzi.
 • Utani au ucheshi unaoweza kuonwa kuwa wenye kuumiza au usiojali hisia za wengine.
 • Maoni ya kutazamia au kuhamasisha mtu au kikundi cha watu kipatwe na madhara.
 • Matusi dhidi ya jamii inayolindwa.
 • Vitisho dhidi ya mtu yeyote au kikundi cha watu, wakiwemo wanasiasi.
 • Picha ambazo zinawaonesha wengine kama wanadamu duni.
 • Kuwalazimisha wengine wakubali maoni yako kuhusu utambulisho maridadi. Kwa mfano, tunachukua msimamo thabiti dhidi ya uaibishaji wa kimwili, au kuwalazimisha wengine wakubali maoni yako kuhusu 'umbo zuri la mwili'.

Unyanyasaji, Mashambulizi au Matusi

Kwenye Chat & Date, Ingawa tunataka ujieleze kwa uhuru unapokutana na yule anayeweza kuwa mwenzi wako, haupaswi kufanya hivyo kwa njia ambayo inaweza kumfanya ajihisi vibaya au kuwa mlengwa wako.

Hupaswi kufanya mambo yafuatayo:

 • Kumfuatilia mtandaoni na nje ya mtandao katika maisha binafsi
 • Kumtumia mtu picha za ngono bila idhini yake
 • Kutoa maoni au unyanyasaji wa kingono usiotakikana
 • Kumtumia mtu bila ridhaa yake picha au video za kimahaba
 • Kujihusisha na unyanyasaji wa kingono mtandaoni
 • Kusafirisha binadamu ili kuwatumikisha kingono
 • Kumshambulia kingono
 • Kuwanyanyasa na kuwatumikisha watoto kingono
 • Kutoa vitisho au matendo ya jeuri

Utapeli, Udanganyifu

Usiwalaghai wanajumuia ya Chat & Date, au kuwadanganya wanajumuia kwa namna yoyote ile ili kujipatia manufaa ya kifedha.

Hii inahusisha:

 • Kuwapa wengine taarifa zako za akaunti ya fedha (Venmo, PayPal, WeChat, nk.) kwa makusudi ya kupokea fedha kutoka kwa mwanajumuia mwingine.
 • Kujaribu kupata taarifa nyeti kabisa kama vile taarifa za akaunti ya benki au namba ya usalama wa kijamii.
 • Kutengeneza fursa ya kulipwa kitu fulani kwa malipo ya pesa au taarifa iliyotumwa.
 • Kutumia mahusiano bandia ya kimapenzi, changamoto za kifedha na/au za kibinafsi ili kujipatia fedha.

Barua Taka

Tunachukulia barua taka kama mazoea ya kutuma ujumbe usiohitajika mara kwa mara kwa makusudi ya kutangaza biashara, sababu zisizo za kibiashara au madhumuni yoyote yaliyokatazwa.

Inahusisha:

 • Maudhui yanayolenga kuvuta uangalifu kutoka kwa watumiaji wa Chat & Date ili kuwaelekeza kwenye tovuti, akaunti, bidhaa na/au huduma za nje.
 • Uundaji wa akaunti nyingi za kupakia maudhui maradufu au kuunda uchumba bandia.
 • Kunakili/Kubandika jumbe za wanajumuia wengine.

Promosheni na Utafutaji

Chat & Date si soko. Kutumia Chat & Date kwa madhumuni ya kibiashara hairuhusiwi. Hii ni pamoja na kutangaza hafla, biashara, muziki, au maonesho yako. Kuomba pia ni marufuku kabisa, hicho ni kitendo cha kuomba, au kujaribu kupata kitu kutoka kwa mtu mwingine au kumwomba mtu afanye kitendo haramu.

Marufuku hiyo inahusisha:

 • Picha inayotangaza huduma au bidhaa zinazouzwa.
 • Kuomba huduma yoyote ikiwemo huduma za ngono na/au ulinzi.
 • Kuajiri burudani ya watu wazima.
 • Viungo vya akaunti za kifedha.
 • Viungo vya maombi.
 • Viungo vya tovuti za kibiashara na/au kutoa taarifa kuhusu huduma yoyote inayotegemea usajili
 • Viungo vinavyoelekeza kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii.
 • Kuomba msaada wa kifedha au zawadi.
 • Kampeni za kisiasa.

Akaunti Maradufu

Ili kufanya Chat & Date iwe yenye kuburudisha zaidi, hatumruhusu mshiriki yeyote kuwa na akaunti zaidi ya moja.

Ikiwa ni pamoja na:

 • Kuwa na akaunti amilifu zaidi ya moja kwa wakati uleule.
 • Kuunda na kufunga akaunti mara kwa mara.

Akaunti za Pamoja

Usiunde akaunti kwa ajili ya kikundi, ukiwa na washirika au marafiki. Chat & Date ni mahali pa washiriki kuonesha uhalisia, wao binafsi.

Jinsi tunavyokadiria

Tunatumia mchanganyiko wa mifumo ya kiotomatiki na timu ya wasimamizi ili kusimamia na kupitia akaunti na jumbe zenye maudhui yanayovunja miongozo hii na Sheria na Masharti yetu. Ikiwa hutaheshimu miongozo yetu au Dhamana ya Unyoofu, msimamizi anaweza kuzuia utumiaji wako wa Chat & Date au kuondoa daima akaunti yako ya Chat & Date (iwe matendo yako yatatokea ukiwa mtandaoni au la).